TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: BENKI YA NCBA YAZINDUA SHINDANO LA NCBA GOLF SERIES 2024 KATIKA KLABU YA ARUSHA GYMKHANA

Shindano la NCBA Golf Series 2024 ilimezinduliwa rasmi leo katika Klabu ya Arusha Gymkhana, na kuleta pamoja jamii ya wapenzi wa gofu na dhamira ya kujenga utamaduni wa michezo huo. 

Benki ya NCBA, taasisi ya kifedha inayoongoza nchini Tanzania, inajivunia kuandaa tukio hili, ikionyesha dhamira yake ya kushirikiana na jamii na kukuza utamaduni mzuri wa michezo. 

“NCBA Golf Series ni zaidi ya mashindano tu,” anasema Bw Claver Serumaga, Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mtendaji  Mkuu wa Benki ya NCBA. 

“Ni fursa ya kusherehekea shauku yetu pamoja kwa mchezo na kuungana na jamii ya Arusha. Tumejitolea kusaidia miradi ya ndani na kuunda athari chanya kijamii, na mashindano haya yanawakilisha dhamira hiyo. 

Shindano hili linaloanzia Arusha linakaribisha gwachezaji wa gofu wa ngazi zote za ustadi, kuanzia wataalamu wenye uzoefu na wapenzi wanaotaka kushindana kwenye uwanja wa  klabu ya Arusha Gymkhana. 

Mpangilio wa uwanja huu unaahidi kupima ujuzi wa washiriki, wakati pia kukuza urafiki na uanamichezo. Zaidi ya msisimko wa mashindano, shindano  hili linanaonyesha kujitolea kwa NCBA kwa uendelevu wa mazingira.

 Pamoja na tukio hilo, NCBA itaanzisha mpango wa upandaji miti jijini Arusha, ikisisitiza dhamira yake ya kuweka mazingira bora kwa kila mtu. Tukio hilo linaahidi siku ya kufurahisha kwa watakao hudhuria. 

Wapenzi wa mchezo wa gofu na washiriki wote wanaweza kutarajia onyesho la talanta ya kipekee ya gofu na roho ya ushindani mzuri.  Mashindano hayo yataendelea mwezi wa Agosti mwaka huu jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake Waziri wa Michezo Damas Ndumbaro alisema- Serikali imeona umuhimu mkubwa wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na mchezo wa Golf kwa namna hiyo Tanzania itaweza kufanya vizuri na kuweza kushindana kwenye mashindano kimataifa kupitia mashindano haya, ndio maana wenzetu wa NCBA waliamua kuliona hili kwa maendeleo ya mchezo huu. 

Pia alisisitiza umuhimu wa uwekezaji kwa kizazi kipya kwa vijana kuanzia mashuleni kwenye mashindano ya umiseta na umishuta na serikali itaweka mpango kuhakikisha mchezo huu unakuwepo mashuleni kuanzia mwakani. 

The NCBA Golf series  washindi ni: Mshindi wa jumla -George Ogutu, mshindi wa kwanza  Division 1  – Jah Nathwani 36, mshindi wa pili Division 1  – Luv Lodhia 35, Mshindi wa kwanza Division 2  – Owen Maganga 40, mshindi wa pili  Division 2  -Jamali Mukarram 39, Mshindi wa kwanza Division 3 –  Dian Vaja 37,mshindi wa pili Division 3 – Bhavesh Gohil 37, Mshindi kwa wafanyakazi wa NCBA  – Claver Serumaga 35, Mshindi wanawake  – Tanvi Kaur Bansal na mshindi wa pili wanawake – Jasleen Kaur

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Damas Ndumbaro (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya mashindano NCBA Golf Series na mshindi wa jumla wa mashindano hayo, George Ogutu (wapili kulia) Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NBCA, Claver Serumaga(wapili kushoto), Nahodha wa Arusha Golf, Sheetal Aggarwal na Mwenyekiti wa umoja wa Golt Tanzania, Gilman Kasiga. Mashindano hayo yalifanyika mwisho mwa wiki kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Arusha

Related Posts