Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe amesema mtu kuwa chama cha upinzani inahitaji ujasiri.
Mbowe ametumia kurasa zake za kijamii kuelezea maisha ya wanasiasa ndani ya upinzani na wale walioko chama tawala. Ujumbe huo unasomeka:
“Kuwa chama cha upinzani hasa Chadema sio suala jepesi, linahitaji ujasiri wa namna ya pekee. Viongozi wengi wa upinzani na Watanzania wazalendo wa nchi hii wanapitia nyakati ngumu kutokana na uoga wa Serikali ya CCM.
“Marehemu Mzee Lowassa alithubutu kuingia Chadema, japo baada ya muda alirudi CCM tunatambua ujasiri wa uamuzi yake. Kitu pekee kitakachoiokoa Tanzania kutoka kwenye mikono ya watawala ni ujasiri na uthubutu wa mwananchi mmoja mmoja; tuanze sasa kulipigania Taifa letu,” ameandika Mbowe jana Jumapili, Juni 30, 2024.
Endelea kufuatilia Mwananchi.