Israel yamwachilia daktari wa Al Shifa miongoni mwa mateka 50 wa Kipalestina
Jeshi la Israel limemuachilia huru mkurugenzi wa kituo cha matibabu cha Al Shifa huko Gaza baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya miezi saba kufuatia uvamizi wa kijeshi katika hospitali hiyo mwezi Novemba mwaka jana.
Dk. Mohammed Abu Salmiya alikuwa miongoni mwa Wapalestina 50 walioachiliwa kuvuka mpaka wa mashariki wa kati na kusini mwa Gaza.
Alikamatwa mnamo Novemba 23 pamoja na wafanyikazi kadhaa wa matibabu wakati wakisafiri kupitia Mtaa wa Salah al Din kutoka Mji wa Gaza hadi maeneo ya kusini ya eneo hilo baada ya jeshi la Israeli kushambulia Hospitali ya Al Shifa.