Wafanyakazi kiwanda cha chai mkoani Njombe wagoma kuingia kazini wakishinikiza kulipwa mshahara wao wa miezi minne

Wafanyakazi wa Kiwanda cha Chai cha Kampuni ya DL Group kilichopo mtaa wa Kibena kata ya Ramadhani mkoani Njombe wakiwemo wachumaji wa majani ya chai wamesimama kufanya kazi na kusababisha shughuli zote za uzalishaji kusimama wakishinikiza kulipwa stahiki zao ikiwemo mshahara wa miezi minne.

Ayo TV imefika kiwandani hapo na kukuta wafanyakazi wakiwa wamekusanyika nje ya geti la kiwanda ambapo wamedai kuwa kutolipwa mshahara wao miezi minne (4) kumesababisha maisha yao kuwa magumu na kushindwa kumudu mahitaji muhimu ya familia ikiwemo kuto peleka watoto shuleni huku pia mtaani wakishindwa kukopesheka.

“Tunataka mishahara yote ya miezi minne na NSSF yetu ya miaka mitano,tumetumika na kudanganywa vya kutosha na tumevumilia lakini sasa uvumilivu umeishia hapa yani tumezua picha mbaya hadi mashuleni wafanyakazi wa kibena ni wasumbufu kutoa michango na tukienda mtaani kukopa wanasema wewe mfanyakazi wa chai hatukukopeshi”Amesema Chesco Mligo.

Aidha licha ya jitihada zizofanyika za kukutana na Meneja wa kiwanda hicho bwana Gerad Ngenzi amesema hawezi kuzungumza lolote kwani msemaji wa Kampuni hayupo katika eneo hilo.

Hata hivyo siku kadhaa zilizopita Mkurugenzi wa Kampuni ya DL Group David Lingat akizungumza wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka alisema kuna changamoto ya biashara ya chai na si katika Kampuni hiyo pekee bali katika sekta ya chai lakini wanaweka mikakati ya kutafuta suruhisho kwa kushirikiana na serikali ili waweze kutatua changamoto.

Related Posts