SERIKALI ya Ukraine imefanikiwa kutibua njama za kuipindua serikali ambayo imekuwa hasimu mkubwa wa Urusi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).
Taarifa iliyotolewa na mtandao wa Telegram imeeleza kuwa, Shirika la Ujasusi la Ukrainme (SBU) ilidai kuwa waandaaji wa mapinduzi walipanga kuzua ghasia jijini Kyiv tarehe 30 Juni 2024 na kudhibiti Bunge la Ukraine na kuondoa uongozi wa kijeshi na kisiasa madarakani.
Taarifa hiyo imeeleza, washukiwa wanne wametambulika huku wawili wakishikiliwa.
Haijabainika iwapo washtakiwa hao wana uhusiano wowote na Urusi, ambayo imefanya uvamizi mkubwa dhidi ya jirani yake huyo wa kusini magharibi kwa karibu miaka miwili na nusu.
Shirika hilo limesema washtakiwa hao wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 ikiwa watapatikana na hatia. SBU ilisema ilikamata silaha na risasi pamoja na simu za rununu, kompyuta na vifaa vingine ikiwa na ushahidi wa hatua za uhalifu.”
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ukraine, kiongozi huyo anayedaiwa kuwa kiongozi wa mapinduzi alikodi jumba lenye uwezo wa kuchukua watu 2,000 na kuajiri wanajeshi na walinzi wenye silaha kutoka kwa makampuni ya kibinafsi ili kuliteka bunge. Haijabainika ikiwa waendesha mashtaka wanatafuta washukiwa wengine zaidi.
“Ili kutekeleza mpango wa uhalifu, mratibu mkuu alihusisha washirika kadhaa-wawakilishi wa mashirika ya jumuiya kutoka Kyiv, Dnipro, na mikoa mingine,” SBU ilisema.
Mpango unaodaiwa kuwa huko Kyiv unakuja wakati Urusi imepata mafanikio kiasi katika uwanja wa vita katika miezi ya hivi karibuni.
Hatua hiyo inakuja wakati Ukraine ikiendelea kutegemea msaada wa silaha za kijeshi kutoka nchi za Magharibi.
Vikosi vya Urusi viliwauwa watu saba, wakiwemo watoto watatu, katika shambulio la kombora katika mji wa kusini wa Vilniansk Jumamosi iliyopita.