Klabu ya Simba imemtambulisha mshambulia Steven Mukwala, raia wa Uganda. kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Asante Kotoko ya Ghana.
Huo ni utambulisho wa tatu kwa Simba kuelekea msimu mpya wa mashindano wa 2024/25 baada ya wekundu hao kumtambulisha winga Joshua Mutale kutoka Power Dynamos ya Zambia na Lameck Lawi kutoka Coastal Union, ambaye hata hivyo ishu yake ilizua utata kwa Wagosi wa Kaya kudai bado beki huyo hajauzwa.
Akiwa Kotoko, Mukwala alifunga mabao 14 na kutoa asisti mbili kwenye mechi 28 alizocheza msimu wa 2023/24 wa Ligi Kuu Ghana.
Mukwala anaenda kuungana na Fredy Michael na Pa Omar Jobe kwenye nafasi ya ushambuliaji ya kikosi hicho.