Dkt. Tulia Ackson atoa salamu za mshikamano baina ya IPU na Jukwaa la Kibunge la SADC

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 2 Julai, 2024 ametoa Salamu za Mshikamano baina ya IPU na Jukwaa la Kibunge la SADC, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 55 wa Jukwaa hilo unaoanza leo Luanda nchini Angola.

Dkt. Tulia anashiriki Mkutano 55 wa Jukwaa la Kibunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-PF) ambao pamoja na mambo mengine, utajadili na kuweka maazimio ya Dhima kuu ya Mkutano huo ambayo ni “Nafasi ya Mabunge kuwa chachu ya matumizi ya Nishati mbadala na safi kwa maendeleo endelevu ya Jumuiya ya Kusini mwa Afrika.”

Katika Mkutano huo, Dkt. Tulia ameambatana na Wabunge Wawakilishi kutoka Tanzania akiwemo Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Shally Raymond, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Mhe. Kassim Haji.

Related Posts