BENKI YA NCBA YAZINDUA MSIMU WA PILI MASHINDANO YA GOFU

BENKI ya NCBA Tanzania imezindua rasmi msimu wa pili wa mashindano ya gofu ya NCBA. Mashindano haya yatafanyika kwenye uwanja wa gofu wa Gymkhana, Arusha.

Akizungumza Wakati wa Mashindano hayo Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Damas Ndumbaro ambaye alihudhuria tukio hilo kama mgeni rasmi, na pia alishiriki katika mchezo wa gofu, aliongelea ushirikiano wake kwa kusema Serikali imefurahishwa kuona Benki ya NCBA ikichukua jukumu la msingi katika kuuinua mchezo wa golfu Tanzania.

“Mpango huu, ukijumlisha na upandaji wa miti sio tu unakuza mchezo wa gofu peke yake lakini inachangia katika juhudi za utunzaji wa mazingira, ikionyesha kuwa michezo inaweza kuleta mabadiliko chanya”.

Aliongeza kuwa Mashindano ya gofu ya NCBA yanalenga kubadilisha mtazamo wa wengi kuona golfu ni kwaajili ya wenye uwezo wa juu na wazee tu, kwa kuwakaribisha wote,ikiwemo wanawake, kujiunga na kushiriki.

Nae Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NCBA Clever Serumaga alisisitiza umuhimu wa ushirikiano huo kati ya Benki na Michezo kwa dhamira moja.

“Kupitia ushirikiano wa mpango wetu wa gofu pamoja na juhudi za upandaji miti, tunaonyesha kujitolea kwetu kwenye mipango ya serikali katika utunzaji wa mazingira”.

aliendelea kwa kusema “Jambo hili linaendana na mpango wa kampuni yetu mama katika kukuza mchezo wa gofu ndani ya Afrika mashariki, kuhamasisha mambo mazuri kwenye jamii, na kutoa jukwaa kwa wachezaji wakubwa wa gofu , na wale wanaochipukia”.
 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwa na Claver Serumaga Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania wakiwa katika hafla ya kugawa zawadi kwenye uzinduzi wa mashindano ya NCBA Golf Series

Related Posts