TETESI ZA USAJILI BONGO: Karaboue asakwa kumrithi Inonga Simba

WAKATI vigogo wa Simba wakihaha kupata saini ya beki wa Cape Town City ya Afrika Kusini, Nathan Idumba ili kuziba pengo la Mkongomani Henock Inonga aliyejiunga na FAR Rabat ya Morocco, inaelezwa pia wanamfuatilia kwa karibu Chamou Karaboue anayekipiga katika Klabu ya Racing Club d’Abidjan ya Ivory Coast.

Beki huyo anatazamwa kama chaguo la pili ikiwa dili la kumnasa Idumba litakwama ingawa bado mazungumzo yanaendelea kati ya pande hizo mbili.

Simba inapambana kusaka beki wa kati baada ya Inonga aliyeitumikia timu hiyo kwa misimu mitatu kuuzwa hivi karibuni huku yenyewe ikiwa katika jitihada za kujenga upya kikosi chake.

Related Posts