EQUITY BANK YAWAKARIBISHA WAJASIRIAMALI KUPATA MKOPO

WAJASILIAMALI na wasambazaji wa bidhaa za kampuni mbalimbali wameshauriwa kufika katika Benki ya Equty Tanzania ili kupata mkopo usiokuwa na riba ili kuendelea biashara zoa.

Meneja Mkuu Biashara, Leah Ayubu ametoa mwito huo jana wakati katika Maonesho ya Biashara Kimataifa Dar es Salaam yanayoendela katika viwanja vya Nyeerer barabara ya Kilwa mkoani Dar es Salaam.

Leah alisema kuwa Benki hiyo itaangalia mauzo ya miezi 12 ya mjasiliamali kutoka katika kampuni ambayo anachukua bidhaa na kupatiwa mkopo bila ya dhamana na bila ya riba.

“Mjasiliamali au msambazaji atapata mkopo wake haraka ndani ya siku moja kwahiyo tunapenda kuwakaribisha waje Equity katika mataei yetu na banda letu hapa katika maonesho kupata huduma mbalimbali” alisema.

Alisema sanjari na mkopo huo kwa wajasiliamali pia Benki hiyo inatoa mikopo ya pembejeo kwa wakulima wa mazao mbalimbali ikiwemo Mahindi, Alizeti.

“Tuna mikakati thabiti kwa ajili ya wakulima kama unavyoona kwenye banda letu tumeweka mitambo mbalimbali ya kilimo kama trekta kwahiyo tunatoa mikopo mbalimbali ikiwemo ya mitaji” alisema.

Alisema kuwa toka mwaka umeanza wametoa mikopo yenye thamani ya Shilingi milioni 46 kwa wakulima wa pamba, Alizeti na mengineyo.

Kwa upande wake mteja wa benki hiyo, Abubakari Ramadhani aliwataka ambao hawajajiunga na benki hiyo kujiunga ili waweze kupata fursa mbalimbali ikiwemo mikopo ya wakulima, na wajasiliamali kutoka katika benki hiyo.




Related Posts