Msanii Dura King aachia EP mpya ‘Inception’, awakonga mashabiki

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

DOUALA, Cameroon – Msanii anayekuja kwa kasi barani Afrika, Dura King, ameendelea kuwapa raha mashabiki zake kwa kuachia albamu fupi mpya, “Inception EP,” kwenye majukwaa yote ya muziki mtandaoni.

“Inception EP” ina jumla ya nyimbo nne kali ambazo ni “Ricky Lover,” “Addicted,” “Lota Love,” na “See Finish,” ambazo zinajumuisha ladha mchanganyiko ya mitindo ya muziki kama vile Afrobeats, Highlife, RnB, na Afropop.

Akizungumza na MTANZANIA DIGITAL, meneja wa Dura King, Rim Plug, alisema mashabiki wameipokea vyema “Inception EP” kutokana na ubunifu wa maudhui ya kijamii na kimila kutoka katika jamii mbalimbali za Cameroon, lengo likiwa ni kuitikisa Afrika.

“Mchanganyiko huu wa kimfumo umeunda sauti nzuri ambayo maelfu ya mashabiki wa muziki wa Dura King hapa Cameroon wamefurahia ‘Inception EP.’ Lengo ni kupenya kila mahali ili kuwapa raha mashabiki wa aina za muziki wa Highlife, Afropop, Afrobeats, na RnB,” alisema Rim Plug.

Aliongeza kuwa sasa mashabiki wanaweza kuingia kwenye mitandao mbalimbali, ikiwa ni pamoja na BoomPlay, kusikiliza nyimbo za EP hiyo kutoka Dura King.

“Inception EP” inatarajiwa kuwa na mafanikio makubwa na kuendelea kumpa umaarufu zaidi Dura King katika tasnia ya muziki barani Afrika.

Kusikiliza gusa link👇
https://www.boomplay.com/share/album/92999207?srModel=COPYLINK&srList=IOS

Related Posts