DKT. ABBAS AWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LA MALIASILI NA UTALII

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas amewaomba wananchi kutembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Maonesho ya SABASABA kwa lengo la Kujifunza na kuona jinsi serikali ilivyofanya jitihada katika uhifadhi.

Ombi hilo amelitoa leo Julai 2,2024 Jijini Dar es Salaam alipotembelea Banda la wizara ya maliasili na Utalii,katika Maonesho ya SABASABA yanayoendelea tangu yalipofunguliwa Juni 28,2024.

Aidha Dkt.Abbas ametoa hamasa kwa  wananchi kujitokeza  ili kujionea wanyama  baadhi ambao wamewaweka katika Maonesho hayo ambapo anaamini watahamasika kwenda hifadhini kujionea zaidi kwa kile watakacho kiona.

“Banda letu litakuwepo kwa siku kadhaa zijazo tunawaomba  sana wananchi waje hapa  Kuna wanyama kama simba,kuna chui,kuna pundamilia,lakini hapa tumeweka wachache ili wananchi wapate tamaa ya kwenda kwenye hifadhi zetu,kwenye mapori ya akiba kujionea kile Mwenyezi Mungu ametubariki Kama taifa”Dkt.Abbas amesema.

Pamoja na hayo,Dkt.Abbas ameeleza kuwa watakao tembelea banda hilo watapata  fursa ya kupata elimu  ya zao la asali pamoja  kujifunza namna  ya kupanda Miche kwa ajili ya matunda na biashara

“Wakati  naingia kwenye Banda letu sehemu kubwa swali langu lilikua wananchi wanauliza nini hasa,utashangaa kuona maswali mengi ya wananchi Ni uwekezaji kwenye eneo la asali na nyuki wafanye nini,wachukue hatua gani kwahiyo hii imetupa picha frani watu wengi wanataka kuhamasika katika biashara ya kufuga nyuki na kuzalisha asali”Dkt.Abbas ameeleza.

Vilevile,Dkt.Abbas amepongeza jitihada za serikali katika sekta ya Utalii ambapo imechangia  kuongezeka kwa idadi ya Utalii wa ndani ambao ni zaidi ya Million 1.5 wakati huohuo ongezeko la watalii wa nje ambao ni million 1.8










Related Posts