Chama aaga Simba | Mwanaspoti

Kiungo fundi wa mpira, Clatous Chama amefunga rasmi ukurasa wake ndani ya Simba SC baada ya kutoa ujumbe wa kuaga kwenye kikosi hicho cha Msimbazi ikiwa ni siku chache tangu kutangazwa kujiunga na watani wao wa jadi na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC.

Chama aliyeitumikia Simba kwa miaka Sita, ameishukuru klabu hiyo na kuitakia kila la kheri.

“Ndani ya miaka sita ya furaha, malengo na kunipa fursa sasa umefika wakati wa kuondoka, sina chochote bali nashukuru kwa heshima na sapoti mliyonionyesha wakati wote tulipokuwa tukiipambania klabu.

“Mmenipa heshima na hakuna atakayebadilisha historia tuliyoiandika pamoja,” amesema.

Chama alitambulishwa rasmi na Yanga Julai Mosi 2024 na kuzua taharuki baada ya kupita siku nzima bila mchezaji mwenyewe kubadili utambulisho wake katika akaunti yake ya Instagram uliokuwa unasomeka ni mchezaji wa Simba SC kabla ya leo kuiweka Yanga SC. 

REKODI ZA CLATOUS CHAMA LIGI KUU BARA AKIWA SIMBA

Related Posts