Chuo cha afya Nobo kuzalisha wataalam wengi wa mionzi

Na mwandishi Wetu

Chuo Cha Afya Nobo kilichopo Tabata Segerea Ilala Jijini Dar es Salaam, kimekuja na mkakatiwa kupunguza uhaba wa wataalam wa mionzi hapa nchini kwa kuanzisha kozi ya fani hiyo.

Mkuu wa Chuo hicho Michael Mbasha , aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba mwakahuu chuo kitafundisha Stashahada ya Uchunguzi wa Magojwa kwa kutumia mionzi ambayo kwasasa kwa nchi nzima haina wataalam wa kutosha.

“Kwa hiyo tutazalisha wataalam wengi wa Utra-Sound na vipimo vingine vya mionzi lengo nikuhakikisha tunasaidiana na serikali katika kuboresha sekta ya Afya hapa nchini.

Mbali na kozi hiyo, pia chuo kinafundisha Stashahada ya Utabibu na Famasia na kwambakitaendelea kuanzisha kozi kutokana na mahitaji ya wataalam.

Anasema kuwa wameamua kuanzisha kozi hizo kwasababu wanaamimi ili uchumi wa nchiuendelee kukua kwa kasi afya kwa raia ni jambo muhuhimu.

“Sasa huwezi kuiachia serikali peke yake ifanye kila kitu, hapana lazima kwa pamojatushirikiane ili kujenga taifa letu.

Anaishukuru serikali kwa kukipa chuo fursa ya kutumia miundombinu yake kama Hospitaliwakati wa mazoezi kwa vitendo.

Anasema kozi zote zitolewazo chuoni hapo zinatambuliwa na taasisi za serikali na kwambamiongozo ya mitihani iko chini ya wizara ya afya.


Mwombaji wa kozi anaweza kuomba chuoni moja kwa moja au kupitia Nactevet.
Kwa mawasiliano zaidi ya Chuo 0744099544

Mkuu wa Chuo Cha Afya  Nobo Michael Mbasha.

Related Posts