Aweso Akagua tenki la kuhifadhi Maji Kibamba saa tisa usiku

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amefanya ukaguzi wa kushtukiza saa tisa usiku katika tenki la kuhifadhi maji Kibamba na kushuhudia maji yakiwa yamejaa ikilinganishwa na hali aliyoikuta juzi tar.1 July alipokuta tenki halina Maji kabisa,

Waziri Aweso amesema kwamba hakuna sababu ya wananchi kukosa huduma ya maji na yaendelee kusukumwa kwa kasi hiihii na kuwataka DAWASA kujidhatiti kauhakikisha hakuna uzembe wala hujuma inafanyika katika kuwafikishia wana Dar Es Salaam Maji safi, salama na yenye kutosheleza.

 

Related Posts