BENKI YA CRDB YASHINDA TUZO YA UBORA WA HUDUMA YA ESQR 2024

Mkuu wa Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Yolanda Uriyo (wa pili kushoto) akipokea Tuzo ya Ubora wa Huduma ya mwaka kutoka kwa Michael Harris, Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Utafiti wa Ubora ya Ulaya (ESQR). Wanaotazama ni Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Tanzania Brussels, Vivian Rutaihwa (wa kwanza kulia), na Meneja Mwandamizi wa Uhakiki wa Ubora wa Huduma wa Benki hiyo, Mshindo Magimba.

 

======   ======

 

 Brussels, 30 Julai, 2024 – Benki ya CRDB

2

imetunukiwa Tuzo ya Ubora wa Huduma kwa mwaka 2024 na Jumuiya ya Ulaya

3

ya Utafiti wa Ubora (ESQR) katika hafla ya utoaji wa tuzo iliyofanyika

4

katika hoteli ya Le Plaza katika jiji la Brussels, Ubelgiji.

Tuzo

5

hiyo ilitolewa kwa kutambua jitihada za Benki hiyo katika kuboresha

6

usimamizi wa ubora katika huduma zake zote. Tuzo ambazo zinafanyika kila

7

mwaka zinatambua taasisi na mashirika ambayo yamewekeza katika huduma

8

ubora kwa wateja katika sekta mbalimbali, ikiwamo sekta ya fedha kote

9

ulimwenguni.

Benki ya CRDB imekuwa ikiwekeza kwa kiasi kikubwa

10

katika mifumo ya utoaji huduma bora inayojumuisha teknolojia za kisasa

11

ili kutoa uzoefu bora katika kila hatua ya safari ya mteja. Ushindi wa

12

tuzo hii, unathibitisha namna gani Benki ya CRDB imekuwa mshirika mzuri

13

kwa wateja na wadau wake, ikichangizwa na wafanyakazi wenye weledi

14

mkubwa ambao wamekuwa wakiwapa wateja suluhisho bora na zinazoendana na

15

mahitaji yao halisi.

Akizungumzia wakati wa hafala ya kupokea

16

tuzo hiyo Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Yolanda Uriyo, alisema,

17

“Mtazamo wetu kubuni njia bora za kuwahudumia wateja umekuwa ndio

18

msingi wa mafanikio yetu ya katika nyanja ya huduma kwa wateja na

19

usimamizi wa ubora. Tuzo hii ni ushahidi wa bidii ya timu yetu katika

20

kutoa huduma bora kwa wateja wetu.”

Aliongeza kuwa tuzo hiyo

21

inaakisi maono ya kimkakati ya Benki ya CRDB chini ya mkakati wake mpya

22

wa muda wa kati, ‘Evolve,’ unaojumuisha mipango mbalimbali ya huduma kwa

23

wateja inayolenga kuboresha utoaji wa huduma. Mipango hii imeimarisha

24

nafasi ya Benki ya CRDB katika soko huku ikiimarisha uhusiano na wateja

25

na ufanisi wa kiutendaji.

Akizungumza kuhusu tuzo hiyo,

26

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema

27

kutambuliwa na ESQR ni hatua muhimu inayosisitiza dhamira ya Benki

28

katika ubora na umahiri katika shughuli zake zote. “Juhudi za timu yetu

29

katika uvumbuzi na mbinu zinazomjali mteja zinaendelea kututofautisha

30

katika sekta ya benki. Tunaendelea kujidhatiti katika kuinua viwango

31

vyetu vya huduma na kutoa thamani endelevu kwa wateja na wadau wetu,”

32

aliongeza.

Mbinu bunifu zilizochangia tuzo hiyo ni pamoja na

33

utekelezaji wa mifumo ya kidijitali ya maoni ya wateja kama vile

34

misimbomilia (QR Code) na mfumo wa jumbe fupi (SMS), zilizopelekea

35

kuwapa wateja njia rahisi za kutoa maoni na kuwezesha benki

36

kushughulikia kwa haraka. Zaidi ya hayo, Benki hiyo imekuwa ikifanya

37

tathmini za mara kwa mara za ubora wa huduma na utoaji wa bidhaa,

Post settings
Labels
No matching suggestions
Published on
7/3/24 3:54 PM
Links
Location
Options

Related Posts