JEAN CHARLES AHOUA NI MNYAMA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Klabu ya Simba imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji Ahoua Jean Charles raia wa Ivory Coast kwa mkataba wa miaka miwili.

Ahoua mwenye umri wa miaka 22 amemsajili kutoka klabu ya Stella Club d’Adjamé ya nchini humo Ivory Coast.

Katika msimu wa 2023/24 Ahoua ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Ivory Coast (MVP) na klabu yake huku akifunga mabao 12 na kutoa ‘assist’ tisa.

Ahoua anasifika kwa kufunga mabao kutoka umbali mrefu, kuchezesha timu pamoja kutengeneza nafasi kwa wenzie.

Simba inategemea mambo makubwa kutoka kwa Ahoua kwa kushirikiana na nyota wengine iliowasajili pamoja na wale waliokuwepo kikosini.

Kuelekea msimu wa Ligi 2024/25 Simba imekuja na utaratibu mpya kwenye usajili wa kuingiza wachezaji bora wenye uwezo na umri mdogo ili kujenga timu imara ya muda mrefu.

Ahoua anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa baada ya Lameck Lawi, Joshua Mutale na Steven Mukwala.

#KonceptTvUpdates

Related Posts