Kabla ya kuanza mkutano huo Putin na Xi wamefanya mikutano ya pembezoni na viongozi kadhaa wanaohudhuria mkutano huo mjini Astana, nchini Kazakhstan.
Viongozi wa nchi wanachama wa SCO watajadili hali ya sasa na matarajio yanayoongezeka katika pande nyingi za Jumuiya hiyo ya na pia nchi wanachama zinataka kuboresha zaidi shughuli za Jumuiya hiyo.
Soma pia: Kazakhstan yataifisha kampuni baada ya mkasa wa moto mgodini
Kabla ya kuanza mkutano huo wa kilele katika mji mkuu wa Kazakhstan, Astana Marais Xi na Putin walikutana na Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan, Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif, na Marais wa Azerbaijan Ilham Aliyev na wa Mongolia Ukhnaagiin Khurelsukh.
India imesema Waziri wake Mkuu Narendra Modi, ambaye anatarajiwa kuzuru nchini Urusi baadaye mwezi huu, hatahudhuria lakini atawakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje Subrahmanyam Jaishankar.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesifu uhusiano kati ya nchi yake na Pakistan alipokutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Shehbaz Sharif kando ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya SCO unaofanyika leo Julai 3 na kesho tarehe 4 huko Astana,mji mkuu wa Kazakhstan.
Soma pia: Shirika la Ushirikiano la Shanghai laikaribisha rasmi Iran
Putin amebainisha kilimo na usambazaji wa nishati kwa Pakistan kama maeneo mawili muhimu ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
“Uhusiano kati ya nchi zetu unaendelea, na uanaendelea kuelekea njia nzuri za kutunufaisha kibiashara. Napenda kuona ongezeko la mauzo ya biashara zetu, na matarajio yetu ni mazuri sana. Juu ya hayo pia ningependa kuzingatia maeneo mawili, ushirikiano wa nishati na biashara inaayohusiana na kilimo.”
Rais Putin na mwenzake wa China Xi Jinping wameliongeza uzito Shirika hilo la Ushirikiano la Shanghai (SCO), lililoanzishwa mwaka 2001 na Urusi, China na nchi zenye nguvu za Asia ya Kati, ambazo zinazijumuisha India, Iran na Pakistan na kuifanya jumuiya hiyo kuwa ni mpinzani wa nchi za Magharibi.
Soma pia: Xi apigia upatu usuhuba wa China na mataifa ya Asia ya Kati
Urusi na China zinaizingatia Jumuiya hiyo ya SCO, kama chombo cha kupambana na vitisho vya usalama wa nje, kama vile uingizaji wa dawa za kulevya na usafirishaji haramu wa binadamu.
Nchi hizo zinawania kupata ushawishi mkubwa kote barani Asia kwa kuonesha umahiri wao katika mbinu za kukabiliana na ukosefu wowote wa utulivu wa ndani.
Vyanzo: RTRE/AFP