Mwenyekiti wa UWT taifa aongoza kongamano la mafunzo ya matokeo ya sensa

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Comrade Marry Pius Chatanda ameongoza Kongamano la Mafunzo ya Matokeo ya Sensa kwa Makundi mbalimbali lililoandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba lililofanyika Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kutoa Mwelekeo wa CCM kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu.

Kongamano hilo lililofanyika wilayani Kahama limejumuisha makundi mbalimbali na viongozi wa chama na serikali wakiwemo Wakurungezi wote wa halmashauri za mkoa wa Shinyanga,Wabunge,Watendaji,mama lishe,na wajasiriamali, waponda kokoto, walimu , manesi na maaskari na watu wenye ulemavu na waalikwa mbalimbali.

 

 

 

 

Related Posts