AWESO ABAINI UZEMBE NA HUJUMA YA MAKUSUDI KWA WATENDAJI WA DAWASA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Waziri wa maji Jumaa Aweso amesema amebaini uzembe na hujuma ya makusudi kutokana na watendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (DAWASA) kutofanya wanayopaswa pamoja na kuzoea kero na malalamiko ya Wananchi.

Amebainisha hayo Julai 3, 2024 alipotembelea Tenki la Chuo cha Ardhi, wilaya ya ubungo Jijini Dar es salaam wakati akieleza mambo aliyo yabaini katika ziara hiyo iliyoanza saa tisa usiku ambapo alitembelea na kukagua miradi kadhaa ya maji jijini humo na mkoani Pwani kwa lengo la kujiridhisha juu ya uwepo wa maji na umeme unaotumika kuendesha shughuli hizo.

Amesema awali wakati akianza ziara yake Juni 29 siku ya Jumapili alitembelea tenki hilo ambalo halikuwa na maji ila sasa maji yapo hivyo amewasihi watendaji hao kutimiza wajibu wao kupitia taaluma zao bila visingizio kwani lengo kuu ni kumtua mama ndoo kichwani.

Aidha, amesema Mamlaka hiyo itakuwa chini ya Wizara ya Maji kwa muda kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo muhimu.

Source; W/Maji

#KonceptTvUpdatesImageImage

Related Posts