Viongozi Ofisi ya Rais-TAMISEMI wakagua miradi Shirika la Elimu Kibaha

Viongozi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wametembelea Shirika la Elimu Kibaha (KEC) kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya elimu pamoja na shamba darasa la ufugaji.

Miradi ambayo yametembelewa na viongozi kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI ni ujenzi wa madarasa matatu katika Shule ya Msingi Tumbi, ujenzi wa darasa pacha katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha na shamba darasa la mifugo. Pia, wageni hao walipata bahati ya kutembelea Shule ya Sekondari Kibaha na Shule ya Sekondari Wasichana Kibaha, Shule ya Sekondari Tumbi na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (Kibaha-FDC).

Viongozi Ofisi ya Rais-TAMISEMI waliotembelea miradi ya maendeleo ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Huduma za Mifumo, Bw. Peter Mhimba na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Emma Lyimo.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaha, Bw. George Kazi mbele ya wageni hao ametoa taarifa ya maendeleo ya shule hiyo kwamba shule hiyo inaendelea kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne na tano katika mwaka 2022 na 2023.

“Shule chini ya Shirika la Elimu Kibaha, tumeweka malengo ya wanafunzi wote kufaulu kwa daraja na kwanza kidato cha nne na kidato cha sita,” amesema Bw. Kazi.

Bw. Kazi amesema kuanzia Julai mwaka huu 2024, Shule ya Sekondari Kibaha imeongezewa tahasusi tatu yaani BUAcCs, ECs M na PMCs. Tahasusi zinaendelea kuwapo ni PCB, PCM, CBA, na ECA.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Tumbi, Bw. Fidelis Haule amewaeleza wageni hao kwamba maendeleo ya kitaaluma yamekuwa yakipanda mwaka hadi mwaka kwa shule hiyo kupata wastani mzuri wa ufaulu katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne na pili kwa miaka yote.

Bw. Haule amesema kutokana shule hiyo kuwa na maendeleo mazuri mwaka 2023, shule hiyo ilizawadiwa shilingi milioni 50 na Makamu wa Rais, Mhe. Isdory Philip Mpango baada ya wanafunzi wengi kupata daraja la kwanza katika mtihani wa Taifa wa kidato cha nne.

Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Haule amesema kuwa kupitia Shirika la Elimu Kibaha, shule hiyo imefanikiwa kufaulisha wanafunzi wote waliorejesha baada ya awali kuacha shule.

“Shule yetu ni kituo cha wanafunzi wa kike walioacha shule kutokana na mazingira magumu na baadaye kuamua kurudi shuleni na kendelea na masomo katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha (darasa la Mh.Dkt. Samia Sululu Hassan).

Naye, Mkuu wa Shule ya Sekondari Wasichana Kibaha, Bi. Felista Mathias mbele ya wageni hao amesema ufaulu umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na walimu wa shule hiyo.wa Huduma za Mifumo kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. Peter Mhimba.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Bw. Robert Shilingi akifafanua jambo kwa viongozi kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI wakati walipotembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika shirika hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bi. Emma Lyimo na kulia ni Afisa Elimu Mkoa wa Pwani. Bi. Sara Mlaki ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. Vicent Kayombo.

Related Posts