Waingereza milioni 50 wanatarajiwa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu leo Alhamisi, huku kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour akitabiriwa kumbwaga waziri mkuu wa sasa, Rishi Sunak, baada ya miaka 14 ya utawala wa chama cha Conservatives. Inaripoti Mitandao ya Kimataida … (endelea).
Uchunguzi wa maoni ya wapigakura unaonesha kwamba Keir Starmer wa Labour atapata ushindi mkubwa kutokana na wapigakura kuchoshwa na wahafidhina, ambao wameonesha kiwango cha juu cha mgawanyiko uliosababisha Uingereza kuwa na mawaziri wakuu watano ndani ya kipindi cha miaka minane.
Hata hivyo, uchunguzi huo wa maoni unaonesha kuwa wapigakura wanataka mabadiliko, na sio kwamba wanakiunga mkono chama cha Labour, kinachofuata siasa za mrengo wa kati kushoto.
Kwenye taarifa yake iliyotolewa leo, Starmer amewaambia wapigakura kwamba huenda leo, Uingereza ikaanza ukurasa mpya, lakini amewaonya kuwa hilo litawezekana tu endapo watajitokeza kwa wingi kupiga kura.