Yamoga nyumba kwa nyumba kushuhudia umeme wa sola ukifungwa kwenye kaya zisizo na uwezo Kilolo

yamoga nyumba kwa nyumba kushuhudia umeme wa sola ukifungwa kwenye kaya zisizo na uwezo Kilolo

Mbunge wa Kilolo, Justine Nyamoga amepita nyumba kwa nyumba kushuhudia namna wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Chuo Kikuu cha The Hong Kong Polytechnic (PolyU) wanavyoshirikiana na vijana wa kijiji cha Magana kufunga umeme wa sola kwenye kaya zisizo na uwezo kiuchumi.

Ufungaji huo wa sola unafanywa na Nyamoga kupitia shirika lake lisilo la kiserikali la VCD.

Baadhi ya wananchi wa kata za Nyanzwa na Mahenge unakofungwa umeme huo wamemshukuru Nyamoga kwa kutimiza ahadi yake hiyo.

“Nguzo ya umeme imepita nyumbani kwangu lakini sina uwezo wa kuingiza ndani, siku zote nilikuwa natumia kibatari lakini leo nitawasha umeme,” amesema Emmaculata Msilu, miongoni mwa wazee kijijini hapo.

.
.
.
.
.

Related Posts