Viwanja vinne kutumika Ligi ya kikapu Mara

MASHINDANO ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Mara yanatarajiwa kuanza Julai 7 mwaka huu, huku katibu mkuu wa chama cha mchezo huo cha mkoa huo, Koffison Pius akitangaza viwanja vinne vitakavyotumika kwa ngarambe hiyo ya kusaka bingwa.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu kutoka Mara, Pius alitaja viwanja hivyo ni Musoma Matumaini, Chuo cha Ualimu Tarime, Nyamongo na Chuo cha Ualimu Bunda. 

Juu ya maandalizi, PIus alisema yamekamilika kwa asilimia zote na kwamba klabu shiriki na wachezaji wameanza kujiweka tayari kwa ligi hiyo.

“Kila kitu kimeenda sawa na timu zitakazoshiriki mashindano hayo zinasubiri kuanza mashindano haya,” alisema Pius.

Alitaja timu hizo upande wanaume ni; Foxes (watetezi), Young Vijana Tarime, Genesis, Hawise, Tour Guide na Waturutumbi.

Upande wanawake timu zitakazoshiriki ni Foxes Divas (bingwa mtetezi), Young vita Queens na Tigress Basketball Club.

Alisema kati ya timu hizo, timu tatu mpya  zinazoshiriki kwa mara ya kwanza ni Genesis Basketball Club, Hawise na Young vita Queens.

Related Posts