TCB yaja na huduma za ubunifu kidijitali maonesho Sabasaba

Benki ya Biashara Tanzania (TCB) ambayo ni moja ya taasisi ya kifedha inayoongoza kwa kutoa bidhaa bunifu za kifedha zinazokidhi mahitaji ya wateja wake, imetoa wito kwa Watanzania kujiunga na huduma za ADABIMA na KIKOBA ambazo zinalenga kuongeza ujumuishi wa kifedha na kuimarisha uchumi na kuongeza pato la Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

ADABIMA ni mpango wa utoaji dhamana wa ada ambao TCB imeshirikiana na kampuni ya Metro Life Assurance ili kuwapa wazazi na walezi utulivu wa kiakili kwa kuhakikisha watoto wanaendelea na elimu yao hata pale wazazi au walezi wao wanapofariki au kupata ulemavu wa kudumu.

Ilihali KIKOBA ni bidhaa mpya, rahisi na yenye ufanisi ya kuweka akiba mtandaoni inayoboresha dhana ileile inayotumika katika vikundi vilivyozoeleka vya kuweka akiba na kukopeshana.

Akizungumzia huduma ya ADABIMA katika banda la maonesho la benki hiyo lililopo kwenye viwanja vya Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba, Mkuu wa Kitengo cha Bima katika benki hiyo, Francis Kaaya amesema wanatambua umuhimu mkubwa wa elimu katika kujenga kesho iliyo bora kwa jamii ya Watanzania.

Amesema ADABIMA inawapa usalama wa kifedha lakini pia inalea ndoto na matarajio ya wateja wake.


“Bidhaa hii ni uthibitisho tosha wa dhamira ya TCB Benki ya kuwasikiliza na kuwahudumia wateja kadiri ya mahitaji yao na kuwahudumia Watanzania wote kwa ujumla,” amesema.

Akielezea kuhusu huduma ya Kikoba, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Bidhaa za Kidigitali kutoka TCB, Pray Henry Matiri amesema huduma hiyo ni zaidi ya fursa ya kidigitali kwa kuwa inabeba dhana pana ya uwazi, ujumuishi na usalama katika uwekaji wa akiba na usimamizi bora wa kifedha.

“Bidhaa hii ya kidigitali na ya kifedha, ikiwezeshwa na ushirikiano wa kimkakati ambao TCB ilifanya na kampuni za simu nchini, inawawezesha wateja kusimamia fedha zao kwa urahisi kutoka viganjani mwao,” amesema.

Amesema ujio wa huduma hizo za TCB katika maonesho hayo, unatokana na wito uliotolewa  jana Jumatano na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mgeni wake Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi aliyetaka washiriki wa maonesho hayo kutumia fursa ya maonesho hayo kujitangaza.

Amesema benki imeimarisha nafasi yake katika ushindani wa soko kwa kutangaza bidhaa zake mpya za kidigitali ambazo  zimebuniwa ili kukidhi mahitaji ya wateja yanayoendelea kubadilika kila maisha ya watanzania ambazoi ni ADABIMA na KIKOBA.

Katika hotuba yake Rais Samia alisisitiza umuhimu wa maonyesho ya Sabasaba katika kuleta maendeleo ya kiuchumi.

Maonesho hayo ya biashara ya 48 yameanza tarehe 28 Juni mwaka huu, yamefunguliwa rasmi jana Jumatano na Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.

Maonesho hayo yameshirikisha zaidi ya nchi 26  na watu zaidi ya 3000 ambao kwa mujibu wa M amlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantred) ni moja ya ongezeko kubwa la washiriki ikilinganishwa na mwaka jana.

Related Posts