TUME ya Ushindani nchini (FCC) imesema itahakikisha Mwananchi nchini haumizwi na bidhaa zisizo na ubora ikiwemo kusimamia sheria ya ushindani nchini inayodhibiti bidhaa hizo.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa FCC, William Erio,wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la FCC lilopo kwenye maonesho ya 48 ya sabasaba yanayoendelea jijini hapa.
Erio amesema FCC imejitahidi kutoa elimu kwa wafanyabiashara juu ya kuepuka Bidhaa Bandia.
“Majukumu yetu pia ni kutoa elimu kwa watu kutofanya Biashara Bandia na kuhalibu ushindani wa biashara,sisi FCC tutaendelea kuchukua hatua”amesema Erio.
Erio,amewataka wafanyabiashara na wawekezaji kabla ya kufanya biashara nchini watembelee FCC kwa lengo la kupata elimu .
“Na sisi tunatumia maonesho haya pamoja na kueleza kazi kwa Umma,tunatumia maonesho haya pia kunawashauri kutofanya Biashara Bandia pamoja kutoweka bei kubwa itakayomuumiza mlaji,”
“Tunawakaribisha kwenye Banda hili ,na sisi tutatoa elimu kipindi chote cha maonesho”Amesema Erio.
Hata hivyo,Erio,amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ni sehemu sahihi kwa uwekezaji kutokana na sera nzuri ikiwemo kuwepo kwa mamlaka inayodhibiti bidhaa bandia ikiwemo FCC.