Msanii wa filamu na muziki nchini, Zuwena Mohamed (Shilole) ametangazwa kuwa balozi wa kampuni ya gesi ya Oryx kupitia shughuli za ujasiriamali wa chakula “Mama Lishe”.
Shilole mwenye mgawaha maarufu wa chakula wa Shishi Food Mama Lishe Zuwena Mohamed maarufu Shilole amepewa jukumu la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia inayozalishwa na kampuni hiyo.
Kampuni ya Oryx imekuwa ikifanya jitihada za kuunga mkono ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia iliyoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2032 zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia.
“Tumeamua kumchagua Shilole kwasababu ni mfano wa kuigwa katika jamii katika shughuli za mama lishe hivyo ataongeza hamasa zaidi kwa mama lishe na baba lishe kutumia nishati safi ya kupikia na kuachana na kuni na mkaa ili kwa pamoja tulinde mazingira yetu na tuhakikishe tunaenda sako kwa bako na Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu katika ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia” amesema meneja mauzo na masoko wa Oryx Gas, Shaban Fundi
Kwa upande wake, Shilole amesema hamasa na jitihada inayofanywa na kampuni ya Oryx Gas katika kuunga mkono malengo ya Dkt Samia ndio chachu iliyomfanya kuridhia nafasi hiyo. Rais Dk.Samia Suluhu ameweka malengo ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya Watanzania iwe inatumia nishati safi ya kupikia.
Cc;Azam Media
#KonceptTvUpdates