Dar es Salaam. Takribani wajasiriamali 1,000 wadogo, wa kati na chini wanakutanishwa katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Juni 5, 2024 kujadili fursa zilizomo katika sekta hiyo.
Wadau wa sekta hiyo iliyoajiri idadi kubwa ya vijana nchini, watakutana katika Kongamano la Wajasiriamali Wadogo, wa Chini na wa Kati (MSMEs), lililoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko atakuwa mgeni rasmi wa kongamano hilo pamoja na viongozi wengine wa taasisi na wakala za Serekali watakuwepo.