Anguti Luis atua Coastal Union, kukiwasha KAGAME CUP

Beki Anguti Luis atakuwa sehemu ya kikosi cha Coastal Union msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Beki huyo kutoka nchini Uganda anajiunga na Coastal Union akitokea KCCA ya nchini kwao, na tayari ametambulishwa na klabu hiyo ya jijini Tanga.

Taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Coastal Union imemmwagia sifa Anguti, ambaye anaaminika anakwenda kuendeleza mazuri katika safu ya ulinzi ya klabu hiyo.

Anguti ana uwezo wa kucheza namba nne na tano ataanza kuonekana akiwa na Coastal Union kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati ‘CECAFA Kagame Cup’ itakayoanza Julai 9, 2024.

Beki wa kati Coastal, Lameck Lawi alitambulishwa kujiunga na Simba, lakini Wagosi wa Kaya waliibuka na kusema dili hilo la uhamisho lilishakufa baada ya Wekundu wa Msimbazi kushindwa kutimiza masharti na hivyo nyota huyo anabaki Tanga. 

Related Posts