WATUMISHI TARURA WAPATIWA ELIMU YA KUJIKINGA NA MAGONJWA YASIYO AMBUKIZA (NCDs)

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Watumishi wa TARURA Makao Makuu wamepatiwa elimu juu ya masuala ya msongo wa mawazo, kupima afya pamoja na ushauri namna ya kujikinga na Magonjwa Yasiyo Ambukiza (NCDs) hususani mahala pa kazi.

Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo Kaimu Meneja wa Utawala na Rasilimali Watu TARURA, Bw. Joseph Sassi amesema lengo la kufanya mafunzo hayo ni kutekeleza sera ya masuala ya UKIMWI na Magonjwa Yasiyo Ambukiza (NCDs) mahali pa kazi.

“Sisi kama watumishi muda mwingi tunakaa ofisini hivyo mafunzo haya yatawasaidia watumishi namna ya kujikinga na magonjwa Yasiyo Ambukiza ili kulinda afya”, alisema.

Amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi na hivyo itajenga mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara na pia kuepukana na magonjwa Yasiyo Ambukiza.

Related Posts