Wanaomkwamisha Samia kuipatia Tanzania katiba mpya, watajwa

Mtandao wa Utetezi wa Haki za Binadamuy Tanzania (THRDC) umesema watu wanaomzunguka Rais Samia Suluhu Hassan ndio wanaomkwamisha kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pia mtandao huo umeeleza kuwa mfumo wa sheria kandamizi pamoja na katiba ya sasa ni chanzo kinachomkwamisha Rais Samia kutekeleza utashi wake katika utetezi wa haki za binadamu kuanzia ngazi ya Serikali kuu hadi za mitaa.

Hatua hiyo inatokana na utashi wa Rais Samia aliouonesha tangu alipoingia madarakani kwa kuondoa vifungo vilivyokuwa vinakiuka haki za binadamu ikiwamo zuio la mikutano ya hadhara na kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa jijini Dar es Salaam kuhusu ripoti ya hali ya watetezi wa haki za binadamu na nafasi za kiraia nchini, Mkurugenzi wa mtandao huo, Onesmo Olengurumwa amesema hatua hiyo inathibitishwa na hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu kuendelea kupungua.

Alitoa mfano kuwa kilio cha mabadiliko ya sheria za habari kimesikika na baadhi ya sheria zimefanyiwa marekebisho huku mfumo wa haki jinai nao ukiwa umefumuliwa jambo linalodhihirisha dhamira ya Rais Samia katika utetezi wa haki za binadamu.

Rais mstaafu Jakaya kikwete na Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein wakiwa wameinua juu Katiba inayopendekezwa katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma tarehe 8 Oktoba 08, 2014. Kulia ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Samuel Sitta akifuatiwa na Makamu wake Samia Suluhu Hassan.

Amesema tatizo limebaki kwa taasisi za utetezi wa haki za binadamu ambazo bado zinakabiliwa na sharia kandamizi ambazo kama sheria ya makossa ya mtandai ya mwaka 2015 kifungu cha 16 ambayo kinamruhusu polisi kukagua simu ya mtuhumiwa jambo ambalo ni kinyume hata na Katiba.

Akieleza sababu za kumsifia Rais Samia katika utetezi wa haki za binadamu, Olengurumwa amesisitiza si kweli kwamba kila mwanaharakati au mtetezi wa haki za binadamu hupingana na serikali.

“Yapo mambo mazuri anayoyafanya lazima tumsifie ili kumjengea utashi wa kukubaliana na sisi yale ambayo tunaona yanakiuka haki za binadamu,” alisema.

Akizungumzia ripoti hiyo yam waka 2023, Olengurumwa amesema kwa mwaka 2023 jumla ya watetezi 100 wa haki za binadamu walisaidiwa kwa uhamisho wa muda mfupi, matibabu, msaada wa kisheria, na usaidizi mwingine wa dharura.

“Jumla ya watetezi 42 walio hatarini (wanawake 6, wanaume 36) walipata usaidizi wa kisheria wa moja kwa moja kutoka THRDC na watetezi 15 miongoni mwao waliachiliwa na mahakama baada ya kushinda kesi au kwa upande wa waendesha mashtaka kushindwa kuthibitisha kesi dhidi ya watetezi wa haki za binadamu waliokuwa kizuizini hivyo kuachiliwa bila masharti.

“Kesi dhidi ya mtetezi mmoja alishindwa na akahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 5 jela au kulipa faini ya Sh milioni saba,” amesema.

Hata hivyo, tarehe 2 Julai 2024 aliachiliwa kutoka gerezani baada ya kulipa faini ambayo mwao waliachiliwa na alichangiwa na marafiki kutoka mtandao X (zamani Twitter).

“Usaidizi wa ulinzi wa dharura katika suala la uhamishaji ulitolewa kwa watetezi 27 (wanawake 3, wanaume 24), msaada wa matibabu kwa HRDS 7 (mwanamke 1, wanaume 6), na familia 6 za HRDS zilipewa usaidizi wa kibinadamu.

“Zaidi ya hayo, watetezi 10 walipewa usaidizi wa rufaa ya dharura kwa mashirika ya nje yanayokuza na kulinda haki za HRDs,” amesema.

Amesema kesi nane za kimkakati zilifadhiliwa katika eneo la uhuru wa kujieleza, makubaliano ya pande mbili, haki za ardhi na haki za wanawake na watoto.

Related Posts