Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya ametembelea banda ya Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, Bw. Mwandumbya alifahamishwa na watumishi wa PPAA kuhusu majukumu ya PPAA ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa moduli mpya ya uwasilishaji wa malalamiko/rufaa kwa njia ya kieletroniki.
Naibu Katibu Mkuu alitembelea banda la PPAA hivi karibuni alipofanya ziara ya kujionea Maonesho ya Sabasaba yaliyoanza 28 Juni – 13 Julai, 2024.