MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA TIB ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA SABASABA

Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania – TIB, Bi. Lilian Mbassy, ametembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amezipongeza Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Fedha kwa kutoa elimu kwa umma kuhusu sera za uchumi na fedha, program, huduma, uwekezaji, benki na masuala mengine kwa umahiri.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania – TIB, Bi. Lilian Mbassy, (katikati), akitembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amezipongeza Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Fedha kwa kutoa elimu kwa umma kwa umahiri.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania – TIB, Bi. Lilian Mbassy, (kulia), akipata Meneja wa Biashara na Uhamasishaji wa Mfuko wa SELF kuhusu Mfuko huo kuwekeza kwa kuwafikia wateja wengi zaidi hususani wa kipato cha chini, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania – TIB, Bi. Lilian Mbassy, (kushoto), akipokea chapisho kutoka Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Main Green Hill ya jijini Dar es Salaam, wakipata elimu kwa wataalamu kutoka Idara na Vitengo vya Wizara ya Fedha kuhusu Sera, Pensheni na Mirathi, bajeti ya Serikali, Mifumo ya Fedha na Usimamizi wa deni la Taifa, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wanafunzi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, wakiwa katika ziara maalumu katika Banda la Wizara ya Fedha, kupata elemu kutoka Vyuo vilivyo chini ya Wizara ya Fedha, wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania- TIB, Bi. Lilian Mbassy, (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Benki hiyo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amezipongeza Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Fedha kwa kutoa elimu kwa umma kwa umahiri.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

Related Posts