WADAU WA USAFIRI WA ANGA WAENDELEA KUTEMBELEA “AVIATION HOUSE” NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA

 

Mjumbe wa Bodi ya TCAA CPA Rukia J. Adam akipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole alipokuwa anaelezea kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga na Mkurugenzi wa Sheria  kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Maria Makalla wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mipango na Takwimu kutoka TAA Edward Kimaro alipotembelea jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba  katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Sheria  kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Maria Makalla akizungumza na Wafanyakazi wa  Baraza la Ushauri la Watumiaji wa. Huduma za Usafiri wa Anga (TCAA CCC) alipotembelea jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA ) Habibu Suluo akipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole alipokuwa anaelezea kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam. Wa Kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga.

akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Uhusiano kutoka TAA Mariam Lussewa alipotembelea jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba  katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga na Mkurugenzi wa Sheria  kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Maria Makalla wakipata huduma katika Banda Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba  katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA ) Habibu Suluo akipatiwa maelezo kutoka Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga kuhusu ndege nyuki (Drone) alipotembelea jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Related Posts