NDEJEMBI AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI – MWANAHARAKATI MZALENDO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka wananchi kuchangamkia fursa za uwezeshaji kiuchumi na mikopo inayotolewa na serikali ili kujiinua kiuchumi na kuchangia katika pato la Taifa.

Mhe Ndejembi amesema hayo jana jijini Dar es Salaam alipotembelea banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake katika maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa ya Sabasaba .

Mhe. Ndejembi amesema kuwa ushiriki wa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake unalenga kutoa uelewa kwa umma kuhusu shughuli inazoratibu na fursa zinazotolewa na serikali ikiwemo suala la uwezeshaji makundi mbalimbali ya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu

Cc:OWM/kvawu

ImageImage

Related Posts