Wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) katika soko la Simu2000 wafunga barabara

Wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) katika soko la Simu2000 Jijini Dar es salaam wamefunga biashara zao na kuweka vizuizi vya kufunga barabara huku wakizuia magari kuingia na kutoka katika kituo hicho cha daladala chanzo kikidaiwa ni kupinga uamuzi wa Manispaa ya Ubungo kukabidhi eneo hilo lenye ukubwa wa mita za mraba 36,000 kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa ajili ya kujenga karakana ya mabasi ya mwendokasi ikiwa ni mbadala wa ile ya Jangwani.

Wafanyabiashara hao wamesikika wakisema hawataki karakana bali wanataka soko lao libaki huku wakiwa wamebeba mabango yanayomuomba Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan awatetee.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko Amefika katika soko la Simu2000 Jijini Dar es salaam ili kujiridhisha ikiwa ni kweli Wafanyabiasha wamefunga biashara zao na kuweka vizuizi vya kufunga barabara huku wakizuia magari kuingia na kutoka katika kituo hicho cha daladala wakipinga uamuzi wa Manispaa ya Ubungo kukabidhi eneo hilo lenye ukubwa wa mita za mraba 36,000 kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa ajili ya kujenga karakana ya mabasi ya mwendokasi

 

Related Posts