Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) kimeendelea kuwa kivutio kwa maelfu ya wananchi wanaotembelea Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) katika maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 48 maarufu kama Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Katika banda la CATC huduma zinazotolewa ni pamoja na maelezo kuhusu kozi mbalimbali za Usafiri wa anga, sifa na faida ya kila kozi. Pia fomu za kujiunga na masomo ya chuo hicho zinatolewa bure kwenye banda la CATC.
Chuo cha CATC ni chuo chenye ithibati za kitaifa na kimataifa kinachotoa kozi za muda mfupi katika upande wa Usafiri wa Anga. Na pia ni Kituo cha Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) katika upande wa kozi za Usalama wa Usafiri wa anga (ASTC-Dar es Salaam) ambapo kwa sasa ni nchi 35 tu duniani ndio zenye sifa hizo.
Afisa Habari na Masoko Mwandamizi Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Ally Changwila akitoa elimu kuhusu namna ya kujiunga na Chuo hicho kwa mwananchi aliotembelea Banda la CATC lililopo katika jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Afisa kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC), Emily Sadock akitoa elimu kwa mwananchi aliotembelea Banda la CATC lililopo katika jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akiendelea kutoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la CATC lililopo katika jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Afisa kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC), Farhat Sadick, kwa wananchi aliotembelea Banda la CATC lililopo katika jengo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (Aviation House) lililopo ndani ya viwanja vya Sabasaba katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.