CPA Makalla ampongeza mwenyekiti na rais Dkt Samia kwa kuboresha huduma za matibabu

Tumekuja kuona jitihada za Serikali na kazi kubwa iliyofanyika ya kuboresha huduma kwa Wananchi wetu wa Kata hii ya Kinyerezi na Jimbo la Segerea wote ni mashahidi tunaposema Maendeleo yanaonekana sio Kwa tochi kama tunavyoona Majengo Makubwa ya Kituo Cha Afya Cha Kinyerezi na wasio amini waje wapate huduma mana ni Maendeleo Makubwa ndio Mana tunampongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wetu Dkt Samia suluhu Hassan kwa kuboresha huduma.

CPA Makalla amesema ” Kwa huduma tulizoziona hapa kwa Vipimo tulivyoviona hapa ni vya kisasa na hali Juu na Magonjwa yote, Operesheni ndogo ndogo zinafanyika,Wodi za wazazi nzuri tumeona kliniki zinavyoendelea na wagonjwa wanavyopata huduma hapa” Kwakweli Kituo Cha Afya Kinyerezi kimekuwa msaada mkubwa sana.

Related Posts