Klabu ya Young Africans Sc imethibitisha kuwa itashiriki katika mchuano wa kwanza wa Kombe la Toyota dhidi ya Kaizer Chiefs FC ya Afrika Kusini utakaochezwa kwenye Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein, Afrika Kusini mnamo tarehe 28 Julai 2024.
Yanga Sc inayonolewa na Miguel Angel Gamondi itakabiliana na aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Nasreddine Nabi ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Kaizer Chiefs kwenye michuano hiyo ambayo pia inatumika kama sehemu ya maandalizi ya msimu mpya.
“Kama Young Africans Sports Club, tumefurahi sana kupata mwaliko huu wa kushiriki michuano ya Toyota Cup 2024. Mechi hii inaendeleza uhusiano kati ya timu zetu mbili kubwa barani Afrika, ambayo ilianza mwaka jana tulipowaalika Chiefs kushiriki maonyesho yetu, mechi ya kirafiki iitwayo 𝐖𝐢𝐤𝐢 𝐘𝐚 𝐌𝐰𝐚𝐧𝐚𝐧𝐜𝐡𝐢. Tumefurahishwa na mwaliko huu na tunaahidi kutoa mechi ya ushindani ambayo itatusaidia kujiandaa kwa msimu mpya wa 2024/25” Rais wa Young Africans SC, Eng. Hersi Said]