Rais Macron akataa Waziri Mkuu wake kujiuzulu

Ufaransa. Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amekataa ombi la Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Gabriel Attal la kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya ya chama chao bungeni.

Attal amewasilisha ombi lake la kujiuzuru baada ya matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge nchini humo ambapo chama chake ambacho pia ni cha Rais Macron kimeshindwa idadi ya viti vya wabunge.

“Muungano wa mrengo wa kushoto wa New Popular Front (NPF) ulipata viti vingi (182), ukifuatiwa na muungano wa Ensemble ambao Macron ni mwananchama wake ulipata viti 163 na kufuatiwa na National Rally (RN) kilichopata viti 143 vya ubunge,” imeandika tovuti ya Skynews.

“Ingawa tulikuwa na matokeo bora mara tatu kuliko ilivyotarajiwa, haimaanishi kuwa ni wengi..Kwa hivyo, kwa uaminifu kwa mila ya Republican, nitajiuzulu kesho asubuhi,” amesema waziri mkuu huyo.

Hata hivyo, Rais Macron amemtaka Attal kuendelea kubakia ofisini, ili kudhibiti hali ya amani kwa muda kutokana na viashiria vya ghasia vinavyoendelea mtaani.

“Waziri Mkuu atendelea kusalia, ili kuhakikisha uthabiti wa nchi katika kipindi hichi,” imesema Ofisi ya Rais Macron.

Katika duru ya kwanza ya kura hizo, Chama cha RN kimeongoza japokuwa katika duru ya pili kilizidiwa na muungano wa NPF.

Wakati hayo yakiendelea, bado hali ya usalama haijatengamaa Ufaransa ambayo inatarajiwa kuwa na Bunge lililogawanyika kiitikadi nusu kwa nusu.

Related Posts