Kabendera, Vodacom uso kwa uso mahakamani leo

Dar es Salaam. Mchakato wa usikilizwaji wa kesi inavyohusiana na kukamatwa kwa mwanahabari Erick Kabendera, aliyoifungua mwanahabari huyo dhidi ya kampuni ya huduma za Mawasiliano Kwa simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Ltd unaanza leo.

Katika kesi hiyo Kabendera anaoimba mahakama hiyo iiamuru kampuni hiyo imlipe fidia ya Dola za Marekani 10 milioni (sawa na Sh28 bilioni) akiituhumu kuwa ndio iliyofanikishwa kukamatwa kwake na askari Polisi, tukio analoliita kutekwa,  na kisha kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi, mwaka 2019.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na Jaji Mfawidhi Salma Maghimbi na pande zote zimeitwa kufika mahakamani hapo leo Julai 9, 2024.

Kwa mujibu wa hati ya wito wa mahakama kwa wadaawa (pande zote) kufika mahakamani, kesi hiyo namba 12799/2024 imepangwa kutajwa asubuhi hii, huku ikiitaka kampuni hiyo kufika bila kukosa na kuwasilisha nyaraka zake ambazo inatarajia kuzitumia katika utetezi wake.

“Fahamu kwamba kesi kesi iliyotajwa hapo juu imepangwa kutajwa kikao cha mwisho cha kupanga usikilizwaji Julai 9, 2024, saa 2:30 asubuhi, mbele ya Jaji Maghimbi inasomesema hati hiyo ya wito na kuongeza:

“Unatakiwa kufika katika mahakama hii bila kukosa na lazima uwasilishe siku hiyo nyaraka zote ambazo unatarajia kuzitimia katika kesi yako.”

Katika kesi hiyo Kabendera anadai kuwa kutokana na matukio hayo amepata madhara ya kiuchumi na yasiyo ya kiuchumi, ya kijamii, maumivu ya kiakili na kimaono, hasara ya kutokufurahia maisha hasara ya maendeleo binafsi na hadhi yake katika jamii na kutokuaminiwa kitaaluma.

Hivyo anaitaka kampuni hiyo imlipe kiasi hicho cha pesa, Dola za Marekani 10 milioni (Sh28 bilioni0 kama fidia ya hasara halisi na riba kwa kiwango cha mahakama (asilimi) kuanzia tarehe ya hukumu mpaka kumaliza malipo yote.

Pia anataka alipwe fidia ya hasara ya jumla kadri mahakama itakavyotathmini, gharama za kesi na nafuu nyingine kadri mahakama itakavyona inafaa.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Related Posts