Dk. Slaa atamani kumchapa mboko Samia

MWANASIASA mkongwe nchini Dk. Wilbroad Slaa amesema angekuwa na uwezo angemchapa fimbo Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu wakati nchi nzima ikiwa imetapaa ya mabango yenye ujumbe ‘mama anaupiga’, kuna wanafunzi wamepangiwa kwenda shule shikizi Monduli ambayo haijapauliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Shule hizo shikizi za sekondari ambazo ni maalumu kwa wanafunzi wa kike waliofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi, zilianza kujengwa mwaka 2021 na Rais Samia kupitia mpango wa fedha za UVIKO 19.

Dk. Wilbroad Slaa

Akizungumza na kituo cha runinga cha Clouds leo Jumanne, Dk. Slaa ambaye pia aliwahi kuwa Katibu mkuu wa Chadema, amesema hata Yesu alipoingia hekaluni na kuwakuta watu wakifanya vitu visivyofaa kwenye hekalu la Mungu, aliwatandika mijeledi na kumwaga vitu hivyo.

“Mimi nakasirika kwa sababu mkiiba hela ya Taifa watoto wanakufa kwa sababu hatuwezi kununua dawa.

“Hata leo nikipata nafasi tena nakasirika na akina Samia nakwenda kuwachapa fimbo kwa sababu Serikali imekiri ina upungufu wa asilimia 60 ya madaktari alafu waziri anatembea na gari ya thamani ya Sh 500 milioni. Ni madaktari wangapi wangetibu?

Akizungumzia changamoto za shule hiyo shikizi huko Monduli mkoani Arusha, Dk. Slaa amesema, “Jana nimesolve matatizo matatu… watoto wamechaguliwa kwenye wilaya, wamepelekwa Monduli, kwenye shule ambayo hata  haijapauliwa. Ndio maana nasema Samia ningemchapa hata sasa.

“Jengo halijapauliwa. Mzazi anapeleka mtoto akijua shule ni nzuri lakini mabango yapo kila mahali na ujumbe ‘amejenga madarasa’! wakati watoto wamefika kwenye shule shikizi, wamelazwa wanne wanne kila kitanda. Tanzania ya leo? Amehoji Dk. Slaa ambaye pia aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden kwa miaka minne.

Related Posts