INEC YASISITIZA USHIRIKIANO KWA WATENDAJI WA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegeke akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Julai 9 na 10,2024 Mkoani Tabora.

Kamishina wa Viapo kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Kundiata Robert akitoa utangulizi kabla ya kuwaapisha watendaji hao wa uboreshaji.

Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri wakila kiapo cga kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri mbele ya Kamishina wa Viapo kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Kundiata Robert (hayupo pichani) kabla ya kuanza kwa mafunzo ya siku mbili kwa watendaji wa uandikishaji ngazi ya Halamashauri mkoani Tabora yaliyoanza Julai 9 hadi 10, 2024 katika Ukumbi wa Mkoa wa Tabora. (Picha na INEC).

Afiza Uhamiaji Wilaya ya Tabora MC, Mkaguzi wa Uhamiaji Muhondo Mashili akitoa mada kuhusu uraia wakati wa mafunzo hayo. 

Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri za mkoa wa Tabora wakiwa katika mafunzo hayo.

Na Mwandishi wetu, Tabora na Katavi
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)
imewataka watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani
Tabora na Katavi kuwa na ushirikiano kati yao, Serikali, Vyama vya Siasa na
wadau wengine wa uchaguzi.
 
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegeke wakati akifungua mafunzo
ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji,
Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi
na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo Julai 9 na 10,2024 Mkoani
Tabora.
 
Mafunzo kama hayo yamefunguliwa pia Mkoani
Katavi na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Jaji wa
Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari na yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji
wa Daftari kwenye mikoa hiyo unaotarajiwa kufanyika tarehe 20 hadi 26,
2024.
 
“Matokeo bora ya zoezi hili yanategemea uwepo
wa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji, Serikali, Vyama vya
Siasa na wadau wengine wa uchaguzi,” amesema Jaji Mwambegele.
 
Jaji Mwembegele amewasihi watendaji hao kuwa
na ushirikiano mzuri na wa karibu na Tume wakati wote wa utekelezaji wa
majukumu yao na ikiwa wanahitaji ufafanuzi au maelekezo yeyote, wasisite  kuwasiliana na Tume.
 
Aidha, Jaji Mwambegele amesema wakati wa
uboreshaji wa Daftari mawakala wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo katika
vituo vya kuandikisha wapiga kura jambo ambalo litasaidia kuleta uwazi katika
zoezi hilo.
 
“Mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa
eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima. Mawakala
hao hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu
yao vituoni,”alisema Jaji Mwambegele.
 
Katika hatua nyingine amesema Tume imetoa
vibali kwa Asasi za kiraia 157 kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura na
waangalizi wa zoezi la uboreshaji 33 watakao tazama zoezi la  uboreshaji.
 
Jaji Mwambegele amesema Tume inasisitiza kwa
Maafisa Waandikishaji kuwa, wanapofika katika maeneo yao, wapewe ushirikiano
kwa kuwa ni wadau muhimu.
 
Mafunzo hayo yanahusisha namna ya ujazaji wa
fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voters Registration
System – VRS) ili waweze kupata uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumia
kwa ufasaha mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha wapiga kura.
 
“Mafunzo haya, yanawajengea umahiri wa
kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kisha nao watatoa
mafunzo hayo kwa Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi
ambao ndio watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni,” alisema Jaji
Mwambegele.
 
Aidha, Maafisa TEHAMA watapatiwa mafunzo
maalum ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiufundi
(Troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga
kura vituoni.
 
Mapema kabla ya kuanza mafunzo hayo,
washiriki walikua kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri.
 
Tume imetangaza uzinduzi wa zoezi la
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika Julai 20, 2024 mkoani
Kigoma ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na kauli mbiu ya uboreshaji ni
“Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi Wa Uchaguzi Bora”.

Related Posts