Kikapu Mara wiki ijayo | Mwanaspoti

UZINDUZI wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Mara umeshindwa kufanyika katika Uwanja wa Matumaini ili kupisha sherehe za makanisa zilizofanyika.

Katibu mkuu wa Chama cha Mpira wa Kikapu mkoani humo,  Koffison Pius alisema baada ya kutofanyika uzinduzi huo  umesogezwa mbele hadi Julai 14.

“Tunaheshimu sherehe za kanisa. Tuliamua kuzipisha kutokana na uwanja huo kuwa ni wa kanisa,” alisema.

Alisema timu walizopanga zicheze hiyo ni North Mara na Genesis ilihali Mwembeni ilipangwa kukipiga na Young Mvita.

Timu zitakazoshiriki ni Foxes (bingwa mtetezi), Young Vijana, Genesis, Hawise, Tour Guide, Mwembeni na Waturutumbi.

Upande wa wanawake ni Foxes Divas (bingwa mtetezi), Young Vita Queens na Tigress.

Related Posts