WAKATI mzunguko wa pili wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) ukianza mwishoni mwa wiki iliyopita, umeonyesha kwamba timu za Dar City na UDSM Outsiders zina nafasi kubwa ya kutoboa kucheza hatua ya nane bora.
Nafasi ya timu hizo itakuja endapo zitashinda michezo saba kila mmoja itakayofanya ziwe na pointi 45 katika mashindano hayo.
Pointi 45 zitatokana na 14 zitakazopata na kuchanganya alama 31 zilizokuwa nazo hadi kufikia Jumapili.
Nafasi nyingine inayoweza ikazinyanyua timu hizo endapo zitapoteza michezo tisa itakayosalia ni kutokana na sheria ya mchezo huo kueleza kuwa timu inayofungwa inapata pointi moja.
Kuongezewa pointi moja itafanya timu hizo ziwe na pointi 54, zitakazofanya zitinge hatua ya nane bora.
Hata hivyo, licha ya timu hizo kushika nafasi za juu, Savio, Mchenga Star, JKT, Vijana ‘City Bulls’, ABC, DB Oratory, Mgulani JKT, KIUT, Ukonga Kings, Jogoo na Srelio nazo zina nafasi ya kucheza nane bora.
Nafasi hiyo ya timu hizo itapatakana endapo zitafanya vizuri katika michezo zitakayocheza.