LICHA ya kupiga chini kucheza mchezo wa ‘mixed doubles’ pamoja na Andy Murray kwenye michuano ya tenisi ya Wimbledon, mwanadada Emma Raducanu ameshindwa kufikia lengo la angalau robo fainali kwenye michuano hiyo baada ya kuondolewa raundi ya nne na Lulu Sun.
Emma ambaye ana taji moja kubwa la tenisi duniani (Grand slam), alipiga chini fursa ya kucheza pamoja na Murray kwenye mchezo uliotarajiwa kuwa wa mwisho kwa Andyz ambaye atastaafu tenisi kwenye michuano ya olimpiki Ufaransa.
Kupiga chini mchezo wa pamoja na Murray ulimfanya mama wa Murray, Judy kuandika kwa hisia jinsi ambavyo haikuwa sawa mwanaye kutocheza mchezo wa mwisho akiwa na Emma licha ya kukiri waliopanga ratiba ndio wanastahili lawama.