Makamu wa Rais akabidhi magari mapya kwa Wakuu wa Wilaya

Ikiwa leo ni siku ya pili ya ziara ya kikazi ya Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, katika mkoa Kigoma na mapema ya leo Makamu wa Rais amekabidhi magari matano kwa Wakuu wa Wilaya Tano za Mkoa wa Kigoma.

Katika kukabidhi magari hayo Makamu wa Rais amewataka wakuu wa wilaya nchini kuhakikisha magari hayo yanatumika kuwahudumia wananchi na hategemei yaonekane sehemu za starehe.

Magari hayo ya Wakuu wa Wilaya yametolewa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya matumizi ya kikazi kwa wakuu wa wilaya, na hafla ya makabidhiano imefanyika Ikulu ndogo iliyopo eneo la Ujiji, Kigoma.

.
.
.

.

Related Posts