DKT. MRAMBA ATEMBELEA BANDA LA CBE SABASABA

Naibu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE), anayeshughulikia Taaluma Utafiti na Ushauri Dk. Nasibu Mramba leo, Julai 09,2024 ametembelea Maonesho ya Kimataifa ya 48 ya Biashara (Sabasaba), na kufika katika Banda la Chuo hicho ambapo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kusikiliza kazi za kibunifu zilizifanywa na wanafunzi wa Chuo hicho.

Dk. Mramba alisema, Chuo hicho kimeboresha mitaala yake hivyo kutoa nafasi ya wanafunzi kujifunza darasani na kwa vitendo.


Related Posts