Bi Beng’ Issa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu Utekelezaji wa Programu ya Kizazi chenye usawa amevitaka baadhi ya Vikundi vya wanawake kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba ili waweze kuoiga hatua katika umoja wao kwani katika uchumi ili upige hatua lazima uweka akiba.
Mjumbe huyo ameyasema hayo katika Ziara ya Kamati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu Utekelezaji wa programu ya Kizazi chenye usawa iliyofanywa Jijini Dodoma Leo July 9,2024, ambapo wajumbe hao wametembelea kikundi cha Wanawake wafugaji wa kuku cha Wining Star kilichopo Ilazo Mbuyuni na Kiwanda cha uchakataji makopo kilichopo Mnada mpya kata ya Kizota nakujionea shughuli mbalimbali zinazoendelea kwa wanawake hao.
Na kuongeza kuwa watakapojiwekea akiba zao wenyewe wanaweza kujenga maeneo yao na kuondokana na kupanga kama ilivyo sasa.
“Nafikiri kitu cha kufanya ni kuendeleza Vikoba vyenu na kikundi chenu muwe na utaratibu wa kuweka akiba ili muweze kuweka pesa yenu wenyewe ili iwawezeshe baadae kujenga iwe mtapata eneo bure au kununua mtaweza kujenga kwasababu mna mradi mnaingiza,tunasemaga katika uchuni ili upige hatua lazima uweke akiba”.
Pia amewataka kuwa na utaratibu wa kutunza taarifa zao kwa kuwa na vitabu ili waweze kuona wanapiga hatua kiasi gani katika mauzo na hata gharama wanazotumia.
“Lakini kitu kingine ni utunzaji wa taarifa zenu sasa,kwasababu huu ni mradi lazima muone kama mnapiga hatua na kwa kiasi gani,hivyo lazima muwe na vitabu mnatunza taarifa za mauzo,gharama na mengineyo “.
Naye moja ya wajumbe walioongozana katila ziara hii ya kutembelea vikundi mbalimbali vya uwezeshaji wanawake kiuchumi Bi Nangi Massawe kutoka Bank kuu ya Tanzania naye amewasihi wanavikundi kuweza kujaribu kutoka na kuona wengine wanafanya nini na kuweza kufikiria kufanya kitu kingine zaidi kutoka katika kile wanachofanya mfano kama wanafuga kuku wa mayai basi wafuge na kuku wa Nyama ili kukuza zaidi miradi yao.
“Sasa katika kwenda mbele zaidi lazima mtoke lazima mtoke mjue huko kwingine wanafanya nini,mmepewa mfano kwa Dar es Salaam wana magroup ya kushauriana katika miradi yao kwa kujua kitu gani kipo na kipi hakipo,na msije mkasimama hapa mnaweza kufikiria kuzalisha chakula ambacho mtatumia ninyi na kingine mkauza”.
Wakati akisoma taari ya kikundi cha winning star kilochotembelewa na Kamati hii katibu wa kikundi hicho Bi Julia Issaya Malaba amesema kuwa kikundi kilianza na mtaji wa Shilingi 6,300,000 ambapo kila mwanachama alichangia 1,050,000 na kuanza kununua kuku 500 ambapo baada ya muda mtaji ulikua hadi kufikia Shilingi 31,250,000 kwa kuku 2500 kabla ya mkopo.
Na kuongeza kuwa walipopata mkopo wa Halmashauri wa milioni 20 iliwasaidia kuboresha na kuongeza kuku 1000 na keji za kuku hivyo kufikia kuku 3500, na mpaka sasa wamefanikiwa kutejesha Shilingi milioni 10,500,000 ndani ya miezi kumi na moja.
“Kikundi kilianza na mtaji wa sh 6,3000,000.00 ambapo kila mwananchama alichangia kiasi cha sh 1,050,000.00 ambazo tulizipata kutokana na kuweka fedha kwenye VICOBA,tukaanza kwa kununua kuku 500 ambapo kwa kipindi cha miaka mtaji wetu ulikua na kuongezeka hadi kufikia sh 31,250,000.00 kwa kuku 2500 kabla ya mkopo”.
“Tuliposikia Mkopo wa Halmashauri wa asilimia nne usio na riba tukaomba mkopo na kufanikiwa kupata milioni 20 mnamo tarehe 30,3,2023 kiasi hicho kimesaidia kuboresha na kuongeza kuku 1000 pamoja na keji za kuku na hivyo kufikia jumla ya kuku 3500 tulizonazo, na mpaka sasa tumefanikiwa kurejesha shiling milioni 10,500,000.00 ndani ya miezi kumi na moja.
Sambamba na hayo pia amegusia baadhi ya changamoto walizoanazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mashine ya kuchakata chakula inayopelekea kuwepo kwa gharama kubwa ya ununuzi wa chakula na pia kuwepo kwa changamoto ya kukosa usafirishaji ambapo amesema watakapoomba mkopo mwingine watakwenda kumaliza changamoto hizi.
“Tunakabiliwa na ukosefu wa mashine ya kuchakata chakula na hivyo kupelekea kuwepo kwa gharama kubwa ya ununuzi wa chakula na ukosefu wa chombo cha usafirishaji,tutakapo kamilisha maresho ya mkopo wetu,tunatarajia kuomba tena ili kukabili changamoto zilizopo”.
Kwa upande wake Mjasiliamali anayemiliki kiwanda cha uchakataji wa makopo ya plasiki kilichopo Mnada mpya kata ya Kizota Bi Aziza Abd Naseeb ametoa Shukurani kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt kwa kuwawezesha Wanawake hapa Nchini pia kwa Mfuko wa Uwezeshaji wa Wanawake ambao ndio walimpatia mkopo wa milioni 100 mwaka 2022 na kubadili historia yake kutoka katika uzalishaji mdogo na kuingia katika uzalishaji mkubwa na kumwezesha kutoa ajira nyingi zaidi kwa wanaume na wanawake ambao ni kutoka 6 alipoanza hadi kufikia 154 kwa sasa.
“Mimi nilianza kwa kuokota makopo momi mwenyewe katika madampo na baada ya miaka 3 nikanunua mashine japo ilikuwa ni ya mkopo na mwaka 2015 nikaanza rasmi kwa ukubwa nikaenda hivyo na mwaka 2022 mfuko wa uwezeshaji wanawake kiuchumi uliniona wakanipa nafasi wakaniwezesha milioni 100 ambapo nilinunua gari na kuondokana na matoroli katika ukusanyaji wa mizigo, hivyo kwasasa nakusanya mzigo kwa haraka ambapo nakusanya mpaka tani 120 kwa mwezi. Poa nina wafanyakazi 154 kutoka 6 niliokuwa nao mwanzo kati yao 46 ni hapa kiwandani na 84 niwa mtaani ninakonunulia mzigo”.
Ziara hii ya Jukwaa la usawa wa kijinsia lilikuwa na lengo kubwa la kujionea shughuli ambazo zimepangwa katika mpango wa Nchi wa kusaidia kukuza usawa wa kijinsia hapa Nchini.