Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) ni moja ya Taasis za Wizara ya Fedha ambazo zinashiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengi ambayo chuo kinaonesha na kueleza ni kozi mbalimbali walizonazo kwa ngazi ya Astashahada (certificate), Stashahada (Diploma), Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) na Shahada ya Uzamili(Master’s Degree) katika fani mbalimbali.
Akiongea na Mwandishi wetu Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa na Masoko, Bi. Sarah Goroi ameeleza kuwa Chuo kinapokea maombi ya kujiunga na Chuo kwa ajili ya Mwaka wa masomo utakaoanza mwezi Oktoba, 2024 na amewakaribisha wahitimu wa kidato cha nne na Sita pamoja na wazazi/ walezi kutembelea banda la IAA ili kuweza kufahamu fursa mbalimbali zilizopo pamoja na kuweza kupata maelezo na ushauri kuhusu kozi zinazofundishwa chuoni hapo.
Banda la IAA liko katika Jengo la Wizara ya Fedha katika maonesho ya 48 ya Biashara maarufu kama Sabasaba.
Spika wa Bunge mstaafu na Kamisaa wa Sensa Anne Makinda akisaini kitabu cha wageni katika Banda la chuo hicho katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Intelejensia ya Jinai CP Charles Mkumbo akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa na Masoko wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Sarah Goroi kuhusu kazi mbalimbali zinazofaywa na IAA alipotembelea banda la chuo hicho lililopo katika jengo la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Kamishna wa Intelejensia ya Jinai CP Charles Mkumbo akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) alipotembelea banda la chuo hicho lililopo katika jengo la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Kaimu Abdi Mkeyenge akisaini kitabu cha wageni katika Banda la chuo hicho katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Kaimu Abdi Mkeyenge akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) alipotembelea banda la chuo hicho lililopo katika jengo la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Afisa Udahili kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Abdalah Mgeleka( wa pili kulia) pamoja na Afisa Uhusiano wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Anord Kavishe (wa kwanza kulia) wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho katika Banda la chuo hicho katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa na Masoko wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda la chuo hicho lililopo katika jengo la Wizara ya Fedha.
Baadhi ya wafanyakazi Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi waliotembelea banda la chuo hicho